Friday, August 12, 2016




MFANO WA MPANZI:

Katika Injili ya Mathayo sura ya 13:4-9
"Hata alipokuwa akipanda, mbegu nyingine zilzianguka karibu na njia, ndege wakaja wakazila; nyingine zikaanguka penye miamba, pasipokuwa na udongo mwingi; mara zikaota, kwa udongo kukosa kina; na jua lilipozuka ziliungua; na kwa kuwa hazina mizizi zikanyauka.  Nyingine zikaanguka penye miiba; ile miiba ikamea, ikazisonga; nyingine zikaanguka penye udongo muri, zikazaa, moja mia, moja sitini, moja thelathini.  Mwenye masikio na asikie."

Yesu  anafundisha kuhusu mfano wa mpanzi wa mbegu ambao ni mfano wa neno la Mungu kama mbegu yake katika maisha ya watu.  Katika kuelewa mfano huu, tunapata mwanga wa kuweza kujua ustawi na Neno la Mungu katika mioyo yetu na pia kujua vitu vinavyoweza kuzuia ustawi wake.  Hivyo pi tunaweza kupata mwanga wa jinsi ya kuomba juu ya Neno la Mungu kwa ajili yetu tupate msaada wake.


MBEGU ZA NJIANI:
Yesu Kristo anatafsiri kuhusu mfano kuwa mbegu zilizoanguka njiani na ndege wakazila nia watu ambao wanalipokeao Neno la ufalme wa Mungu wasilielewe naye yule mwovu akalinyakua lililopandwa moyoni mwake.

Kuna umuhimu mkubwa wa watu kupata uelewa wa Neno la Mungu, kuanzia yule alisemaye kwa watu, na pia wale wanaolisikia Neno hilo na kulipoke ili mwovu asiweze kuliiba neno hilo toka kwao. Kwa sababu neno hilo la Mungu laweza kuwa neno la tumaini au neno la uponyaji au liwe neno la kutubu; hivyo kama shetani akiweza kuliondoa kwa sababu mtu huyo aliksa uelewa wa neno hilo, basi halitozaa matunda kwa sababu halitokuwa nae tena.  Hivyo ni jambo la msingi sana wa tu wa Mungu kuomba juu ya yafuatayo:
  • Nguvu ya Mungu katika uelewa wa Neno lake takatifu, pia katika uelewa huo, watu wa Mungu waombe juu ya Uhuru wa fikra na fahamu za watu ili wasiwe wagumu katika kuelewa neno la Mwenyezi Mungu.
  •  Kusimama kinyume katika dhidi ya mashambulizi ya Adui kwa watu wa Mungu katika kuliiba neo la Mungu kwako na kuwafanya wawe wapotofu na viziwi na Neno la Mungu kwa sababu hawaoni likizaa katika maisha yao.
  • Kumwomba Mungu katika kuwafanyia watu hawa mioyo mipya ya maisha yao ili wasiwe watu wa njiani ambao hupitwa nakushambuliwa na adui wa wokovu wa Mungu.
  • Kuomba Mungu awazungushie ulinzi wake watu hawa na mioyo yao ili wawe na usalama wa neno apandalo ndani yao liweze kuzaa matunda.
Hivyo watu wenye mioyo ya njiani wazidi sana kumtafuta Mungu katika kuzidi kumjua na kumwamini Yesu Kristo nao wokovu wao utakamilika daima na milele katika jina la Yesu kristo.


MBEGU ZA MIAMBA:
Katika ufafanuzi wa mfano wa mpanzi kuhusu mbegu zilizopandwa katika ni wale watu ambao hulipokea neno la Mungu kwa furaha, lakini kwa sababu neno linakosa mizizi ndani yake, linadumu kwa muda tu.  Ila ikitokea dhiki au udhia kwa ajili ya lile mtu huyo huchukizwa na kugeuka moyo kuliacha neno hilo.

Watu hupitia ugumu wa namna hii katika kustawi kwa Neno la Mungu maishani mwao kwa sababu ya ugumu wa mioyo yao.  Watu wa namna hii wanahitaji maombi ya ukombozi sana kwao , lakini pia wanahitaji malezi ya karibu ili waendelee kuelewa zaidi kuhusu Mungu na Kristo wake akiyetupa ulimwengu tuokolewe.  Watu ambao wana ugumu kama miamba katika kuzaa matunda ya neno la Mungu wana tabia zifuatazo.
  • Majivuno.  Watu hawa ni wagumu kujishusha mbele za Mungu, wala kunyenyekea kwao ni kugumu pia.  Ni katika kunyenyekea mbele za Bwana Yesu Kristo ndipo kutakapowaweka huru nafsi zao, na hapo wataweza kuanza kuzaa matunda pia.
  • Shingo Ngumu.  Hapa ni kuhusu watu kushindwa kuacha mambo ya kale, kushindwa kuacha dhambi na pia kujiona kuwa wapo sawa katika kila jambo, hata kama wakikoseana na watu wengine, wao huwa wagumu kusamehe au kuomba msamaha.  Shingo ni ishara ya kukataa Utiisho wa Nguvu Ya Mungu katika maisha yako.
Kwa kufuata mwenendo wa Roho Mtakatifu wa Mwenyezi Mungu (Wagalatia 5:16-26), ndipo wataweza kuishi katika uhuru na kuweza kuyafanya mazuri yaletayo matunda ya Neno la Mungu liishilo ndani yao.


MBEGU ZA MIIBA:
 Katika mfano wa mpanzi, Yesu Kristo anaelezea kuhusu mbegu zilizoanguka katika miiba kama vile mtu aliyepandwa katika miiba ila kutokana na shughuli za Dunia na udanganyifu wa mali, Neno la Mungu ndani yake halizai kutokana na msongamano wa vitu hivyo maishani mwake.

Watu wanaosongwa na miiba wanashindwa kuachia shughulli za maisha yao ya kila siku ili wajitoe katika kutumika katika Yesu Kristo.  Hivyo wanshindwa kuzaa matunda kwa sababu wanaona kumtumikia Mungu kwa kuacha vitu vyote maishani mwao ni Upotofu, au wanaona kuwa wanaweza kumtumikia pamoja na mali zao pia.  Watu hawa wanaweza kuwa sifa zifuatazo:
  • Elimu kubwa na Nafasi kubwa katika maisha yao na jamii inayowazunguka pia.  Hivyo waogopa kupoteza utajiri na heshima ambayo wamejijengea katika maisha yao.
  • Wanasifiwa na watu wengi kwa yale ambayo wameyafanya maishani na katika jamii.  Wanapata utukufu toka kwa watu wengine katika mambo waliyoyafanya duniani, hivyo kuyatelekeza hayo kwa ajili ya Yesu Kristo inakuwa vigumu sana kwao.
  • Wasemaji Wakuu katika Jamii.  Watu hawa wanaweza kuwa na nafasi kubwa za kuwafanya watu wawasikilize katika yale wanayosema.  Wanashiriki vikao vikubwa na wakuu na wana wafuasi wengi wanaowapenda wao na kupenda kazi zao pia.  Wamejivunia utajiri katika hayo yote na hivyo kuyaacha inakuwa vigumu sana kwao.
Watu hawa wanahitaji msaad awa Mungu ili waweze kuwa huru na mambo yanayowazunguka, ni katika upendo mwingi na neema kuu ya Mwenyezi Mungu ndipo watu hawa watapokea Uhuru wao katika Kristo, hivyo ni muhimu sana kuomba Mungu akutane nao katika maisha yao ya kila siku na kuleta mabadiliko.  Ni vema kuomba Mungu aishinde hofu ifunikayo mioyo na fikra zao, kwa sababu wengine wanaogopa kukana shughuli hizo wakiogopa mikataba yao ya Gizani na yule shetani, mwovu au wakiogopa kifo walichoahidiwa kama wakimkana shetani na kumfuata Yesu Kristo.


MBEGU ZA UDONGO MZURI:
Katika mfano wa mpanzi, Yesu Kristo anafafanua kuhusu mbegu zlizoanguka katika udongo mzuri, kama vile watu walisikiao Neno la Mungu, wakalielewa na kulishika, hivyo wao huzaa matunda kwa viasi vyao.   Katika kundi hili, watu wa Mungu ni wa le wawekao bidii katika Neno la Mwenyezi Mungu ndani yao ili liweze kuzaa matunda katika maisha yao ya kila siku.

Watu hawa wanapata uelewa wa Neno la Mungu na linadumu mioyoni mwao.  Watu haw ni wanyenyekevu na pia ni watulivu mbele za Bwana.  Wanao ulinzi wa Mungu dhidi ya Jua na Miiba ya ulimwengu huu, kwa sababu kama vile walivyo katika udongo mzuri, Mwenyezi Mungu amewatenga watu hawa na miyo yao mabali na mambo yanayozuia Ustawi wa Neno lake ndani yao, na mioyo yao pia siyo miamba migumu tena, ndiyo maana ni waelewa wa neno la Mungu na wanaweza kuliishi na kulifuata daima.

Watu hawa wanafuata mwongozo wa Roho Mtakatifu katika mienendo ya maisha yao.  Pia ni washindi dhidi ya mashambulio ya Adui mwovu katika kuwanyang'anya Neno lililo ndani yao kwa maana Mungu yupo pamoja nao wote watembeao katika Njia ya Yesu Kristo daima.

Mtu akiishi katika mfano wa mbegu za Udongo mzuri, ni kwamba anishi maisha yayompendeza Mungu, na ni dhairi kuwa yupo Imara katika maombi mbele ya Mungu na anadumu katika kukua na kustawi mbele ya Mungu kwa mbegu za Neno la Mungu ndani yake. 
Watu hawa wanatabia zifuatazo:
  • Wanadumu katika kutafakari Neno la Mungu maisha yao yote mchana na Usiku.(Zaburi 1)
  • Wanadumu katika maombi bila kukoma ila kuweza kupata Msaada wa Mungu kila siku.(Efeso 4).
  • Wapo Imara dhidi ya vita vya Ufalme wa Giza wakivaa silaha zote za Mungu (Efeso 4).
  • Wanaenenda katika Roho Mtaaktifu na siyo katika mambo ya kidunia(Wagalatia 5).
Watu waaminifu wa Mwenyezi wanayo matumaini juu ya kile walichoahidiwa na Mungu katika Neno la Mungu, ikiwa ni Uzima wa milele na Ufalme wa Mbinguni na pia Mateso ambayo yote ni katika njia ya Uzima na Ukweli na  kumtukuza Mwenyezi Mungu.


NAOMBA USHIRIKI SALA HII:

"Mungu Mwenyezi nashukuru kwa muda ambao umenipa duniani, naomba kwako unijalie uelewa wa Neno na Kweli yako. Naomba unijali kustawi katika kukujua na kukuamini wewe ili nidumu nawe.  Nifunulie zaidi kuhusu mwanao Yesu Kristo na Nuru yako iongoze maisha yangu daima katika Jina la YESU KRISTO...AMINA."


NASHUKURU SANA KWA KUCHUKUA MUDA KUSHIRIKI NENO HILI.  MUNGU AKUJALIE UELEWA MWINGI NA AKUBARIKI DAIMA KATIKA JINA LA YESU KRISTO, NA NURU YAKE IANGAZE JUU YAKE DAIMA...AMINA.

1 comment:

  1. Muache Mungu apande mbegu za neno lake maishani mwako nawe utapokea mbadiliko makuu ya Wokovu wake...Mbarikiwe wote kwa jina La Yesu Kristo.

    Nawe pia waweza weka msemo wa mguso wa Neno la Mungu kwako hapo.

    ReplyDelete

Categories

Powered by Blogger.

Popular Posts