Friday, April 29, 2016


VITU NA WATU WALIOMGUSA MUNGU.
  Tunaposema mwanamke alligusa mavazi ni kwasababu kuna vitu na watu ambao Yesu anawatumia kama mavazi yake,ikiwa umefanya vitu kwao wakafurahi unaruhusu nguvu ya Mungu ipitie wao na kubadilisha maisha yako,ninaposema hayo nina maana hii si kila mtu au kila kitu kimemgusa Mungu,kwamaana hii kuna wengine unaweza ukawagusa kama vazi la Yesu na nguvu za Mungu zisikuhudumie lakini kuna vitu na watu wengine wao wamegusa ngozi ya Yesu ukiwagusa hao hutokuwa kama vile ulivyokuwa ambao ni:

                            i. Watumishi wa Mungu.

Watumishi wa Mungu ni mavazi ya Yesu ndiyo waliomgusa Yesu wao wamebeba mabadiliko ya maisha yako ninaposema kugusa nina maana hii ukionesha kuwajali,  kula pamoja nao,watu wengi wanatamani kuguswa na nguvu ya Mungu wakiwa wamesahau kwamba.
           1Wafalme 17:13-16
“Eliya akamwambia usiogope,enenda ukafanye kama ulivyosema,lakini unifanyie kwanza mkate mdogo uniletee,kisha jifanyie nafsi yako na mwanao.Kwakuwa Bwana Mungu wa Israeli asema hivi,lile pipa la unga halitapungua wala ile chupa ya mafuta haitaisha,hata siku ile Bwana atakapoleta mvua juu ya nchi,Basi akaenda akafanya kama allivyosema Eliya,na yeye mwenyewe na Eliya na nyumba yake wakala siku nyingi.Lile pipa la unga halikupunguka wala ile chupa ya mafuta haikuisha,sawasawa na neno la Bwana kwa kinywa  cha Eliya”
     Mungu alitaka kubadilisha maisha ya mwanamke mjane maana alikuwa amekata tamaa kwasababu ya njaa ya kipindi kile lakini kanuni ya kiroho inasema uviguse vilivyomgusa.Eliya mtumishi wa Mungu alikuwa amemgusa Mungu katika utumishi wake hivyo alikuwa ni vazi la Mungu mwanamke mjane alipofuta njaa kwa Eliya naye Mungu akafuta njaa kwa mwanamke mjane,unapobadilisha maisha ya watumishi wa Mungu naye Mungu anabadilisha maisha yako maana wao wamemgusa Mungu,mwingine anaweza kusema mbona ninacho kidogo mwanamke mjane hakuwa nacho kingi ila alitoa kwa imani na  Mungu akatengeneza mipenyo.
        Si mwanamke mjane tu hata mwanamke mshunemu ambaye alikuwa tasa hazai,lakini alimpokea Elisha na kumpa chakula nakumfanyia kitanda kizuri kwaajili ya kulala bali Elisha ni mtumishi wa Mungu,vazi la Mungu amemgusa Mungu katika utumishi wake,alipompokea Elisha naye akapokea mtoto(2wafalme 4:8).Kumbuka kitendo cha mwanamke kugusa upindo wa vazi la Yesu msiba wake ulipona Gusa vilivyomgusa.
   Hata Ibrahimu Baba wa imani alikuwa amehaidiwa na Mungu kupata mtoto kwa muda mrefu sana lakini asipate,siku moja aliwapokea watumishi wa Mungu walipopita karibu na hema yake na kuwanawisha miguu na kuwapa chakula walitamka kitu kwake “Mwaka kesho wakati kama huu utapokea mtoto”(Mwanzo 18:1-10) akampokea Isaka,wapo wengi waliogusa vilivyomgusa na maisha yao yakabadilishwa,Mungu nataka akuguse na nguvu yake gusa kwanza vilivyo mgusa.


                            i.Makanisa na huduma

Makanisa na huduma mbali mbali ni vitu vilivyomgusa Yesu unapogusa ni lazima maisha yako yabadilishwe,Sulemani alimjengea Mungu nyumba,kwasababu alikuwa amegundua siri hii kwamba nyumba ya Mungu imefungamanishwa na nguvu ya Mungu na alikuwa anataka ufalme wake uwe imara alimjengea Mungu nyumba,haijawahi kutokea katika Israeli mtu aliyekuwa kama Sulemani katika ufalme wake kipindi chake hakujawahi kutokea vita,alikuwa na mahali nyingi kupita  wafalme wote duniani,alikuwa na hekima isiyoelezeka kwasababu alimjengea Mungu nyumba,angalia makanisa yanayojengwa toa mchango wako uone kama nguvu ya Mungu haijakugusa siyo mpaka mchango utangazwe kanisani ndipo  ufanye uonapo tu kuna upungufu fanya haraka ili Mungu aachilie nguvu ya kukugusa,angalia ndani ya kanisa ukiona jengo limechakaa angalia washirika utawaona nao pia wamechakaa,ukikuta kanisa limejengwa vizuri  limepambwa utakuta pia washirika wanamaendeleo kwenye maisha yao.Kwanini? ni kwasababu watu wengi hawajaigundua siri hii.
     Na hata wakati mmoja wazee wa Israeli walimwendea Yesu kwa kumtaka amponye mtumwa wa akida mmoja ambaye alikuwa hawezi,ili maombi yao yajibiwe yawe na ushawishi mbele za Yesu,walionyesha kile alichokifanya kwenye lile taifa,wakasema alitujengea na Sinagogi Yesu akapata ushawishi kwenda kumponya(Luka 7:1-6) unaweza ukawa unataka uponyaji lakini hauja ushawishi ufalme wa Mungu uachilie nguvu yake,wanao jenga makanisa nakusapoti huduma mbalimbali wanakuwa wamegusa vilivyogusa ufalme wa Mungu hivyo nguvu za Mungu zinapita kwenye huduma na kugusa maisha yao,labda hauna kazi,au unafanya biashara bila faida bali unaona madeni yanakuwa mengi,ukiona kunaujenzi wa kanisa nenda ukachangie ili uone kanuni hii ya kiroho inavyofanya kazi.


                            i.Yatima,wajane na mgeni pamoja na maskini.

Watu wengi hawajajua kwamba yatima na wajane,wageni pamoja na maskini wao ni maskini wao ni mavazi ya Yesu kwamba ukimaliza shida zao naye Yesu anamaliza za kwako,kumbuka kile kitendo cha mwanamke mwenye kutokwa damu kugusa upindo wa vazi la Yesu nguvu za Mungu zikamhudumia,Je umewahi kuapata historia ya mwanamke Dorkasi ambaye aliumwa mpaka akafa,kipindi cha uhai wake alikuwa anawajali wajane,angalia mstari huu.
   Matendo 9:39.
“Petro akaondoka akafuatana nao,alipofika wakampeleka juu orofani wajane wote wakasimama karibu naye,wakilia na kumwonyesha zile kanzu na nguo alizoshona Dorkas wakati ule alipokuwa pamoja nao”
    Soma na uelewe tabia ya mavazi ya Yesu ,hawa wajane walisimama kama mavazi ya Yesu,wakatoa sauti za kilio,vile vilivyomgusa Yesu vina sauti inayogusa nguvu inayogusa kwa wakati huo Dorkasi alikuwa hajililii lakini wajane walilia(mavazi yalilia)unaweza ukapita kwenye hali ngumu kwa kiwango ya kwamba ukashindwa kujiombea mwenyewe lakini vile ulivyowahi kuvigusa vilivyomgusa Yesu vikatoa sauti kwaajili yako,kufufuka kwa Dorkas hakukuwa kwa sababu Petro anaoupako wa kufufua wafu ila ni kwasababu Dorkasi amegusa vilivyomgusa.
           Mambo ya walawi 19:9-10
“Na mtakapovuna mavuno ya nchi yenu,usivune kabisa kabisa pembe za shamba lako,wala usiyakusanye masazo ya mavuno yako.Wala usiyakusanye masazo ya mizabibu yako yaliyopukutika uyaache kwaajili ya maskini na mgeni,mimi ndimi Bwana Mungu wako”
      Anaposema utakapoyavuna mavuno ya nchi anamaana hii kila kazi ya mikono unayoifanya ziwe ni biashara,pale ofisini pako haijarishi ni kazi gani kwa kile unacho kipata mahali hapo usisahau vile vinavyomgusa Yesu yaani maskini na mgeni,anaposema maskini anamanisha muhitaji anaposema mgeni ni Yule mtu aliyefikiapo kwenu mfano mfanyakazi wa ndani huyo ni mgeni uanapofanya kwaajili yake unakuwa umevigusa vilivyo mgusa Yesu,wengi wanawanyanyasa wageni yaani wafanyakazi wandani wasijue kwamba wamemgusa Mungu,angalia kile kilichomgusa Mungu kikinung’unika kwaajili yako maisha yako yapo hatarini,usiwasahau wajane yatima na maskini na mgeni.


                            i. Wazazi(Baba na Mama)

Wazazi ni mavazi ya Yesu wamegusa ngozi ya Yesu,hivyo wamefungamanishwa na nguvu ya Mungu,kuna mahali huwezi kufika ukiwa hujafanya kitu kwao,watu wengi wamefanikiwa lakini ukiangalia wazazi wao wanaishi katika hali mbaya,shida,umaskini, hawajui ya kwamba masononeko ya wazazi wao ni mikosi kwenye maisha yao,ili nguvu ya Mungu ikuguse nilazima uviguse vilivyomgusa hii ndiyo kanuni ya kiroho.Isaka alipoona kwamba umri wake umekwenda na macho yake yamepofuka akatakakumbariki mwanawe Esau lakini Isaka Babaye alijua kanuni ya kiroho kwamba Esau asipo vigusa vilivyomgusa hawezi akapokea Baraka za wazazi,hivyo akamwagiza amtengenezee chakula kitamu namna ile anapenda.
     Mwanzo 27:3-4
“Basi naomba chukua mata yako,podo lako naupinde wako,ukaende nyikani uniwindie mawindo.ukanifanyie chakula kitamu namna ile nipendavyo,ukaniletee ili nile Roho yangu ikubariki kabla sijafa”
   Wazazi wako wanataka ufanye kitu kwao kabla hawajafa,wengine wazazi wao wanaishi kwa shida na huku uwezo wanao ila wakifa wanapamba vizuri majeneza ilikuwaonyesha kwamba wanawajali,usijali maiti iliyokufa wajali wazazi wako wakiwa hai ili nguvu ya Mungu ikuguse,Isaka alimwambia shituka Esau nguvu za Mungu haziwezi kukugusa nikiwa nimekufa hata ukinifanyia jeneza zuri kiasi gani nikiwa hai fanya chakula kitamu kama nipendavyo nikubariki.Huwezi kupiga hatua yoyote kwenye maisha yako kama hujafanya kitu kwa wazazi wako,naye mtume Paulo hawi mbali kwamba kuna watu wanakufa leo kwasababu hawaaeshimu wazazi wao.
       Waefeso 6:2-3
“Waheshimu Baba yako na Mama yako;amri hii ndiyo amri ya kwanza yenye ahadi,upate heri ukae siku nyingi katika dunia”
Ni ukweli Mungu amehaidi kwamba miaka yetu ni sabini au tukiwa na nguvu themanini lakini ahadi hiyo ili itimie kwako ni lazima kwanza uviguse vilivyomgusa wazazi ukiwaheshimu wamefunga manishwa na nguvu yakuwafanya watu waishi maisha marefu.Kuna ndugu mmoja alikuafa.Kipindi cha uhai wake alikuwa na kazi yake nzuri,nyumbani kwake alikuwa amejijenga sana lakini alikufa katika umri mdogo sana hata miaka 30 hakufikisha,siku ya mazishi yake ilipofika walienda kumzika mahali alipozaliwa,watu walipotazama maisha ya wazazi wake,maana wazazi wake mahali tu wanapolala,nyumba wanayoishi imejengwa kwa mianzi na kila mmoja akawa anashangaa kwamba yeye aliishi kwenye maisha ya kifahari ia wazazi wake wanaishi kwenye maisha kama haya si angewabadilisha na wazazi wake?kumbe ndiyo maana amewahikufa,unapofanikiwa usiwasahau wazazi wako iliusiondoke mapema duniani wazazi wamebeba Baraka ya maisha marefu,namna unavyowagusa kwakufanya namna wanavyopenda wao,unakuwa sawasawa na mwanamke mwenye kutokwa damu alipovigusa vilivyovyomgusa Yesu aliongeza maisha ya kuishi duniani pamoja na kwamba alikata tamaa.

0 comments:

Post a Comment

Categories

Powered by Blogger.

Popular Posts