Tuesday, May 10, 2016



Umewahi kujiuliza ni kwanini kuna watu wakienda mbele za Mungu wanapokea na wengine, hawapokea ?,Yumkini mara nyingi sana unatamani Mungu akutane na wewe mara tu uendapo hemani mwake, kweli kabisa mahili alipo weka kumbukumbu la jina lake ndipo mahali ambapo Mungu huwabarikia watu wake na kuwaponya magonjwa yao.

Kutoka 20:24
"Kila mahali nitakapotia ukumbusho wa jina langu, hapo ndipo nitakapo kujilia na kukubarikia."


Kumbe ni haki yako Mungu anapobadilisha maisha yako mahali ambapo amepachagua aliketishe jina lake, haiwezekani ukawa ni muhudhuriaji mzuri wa mahali ambapo jina la Mungu limekaa na maisha yako yakawa vilevile, ukiona hivyo ujue kosa si la Mungu, kuna vitu wewe mwenyewe hujaviweka sawa mbele za Mungu, Mungu anataka kila uhudhuriapo mbele zake maisha yako yageuzwe, usiwe kama vile ulivyo lakini wewe toka umeanza kusali sasa ni miaka mingi, lakini maisha yako yapo vilevile, hatuoni Baraka ambazo, Mungu amewahaidi wampendao kwenye maisha yako, kumbuka umaskini si fungu lako, madeni si fungu lako wewe ni mtu unayeshinda mbele za Bwana.Ni kwa muda mrefu sasa ugonjwa ule ule unaumwa na kila siku unapita mbele kuombewa wala hupokei, huoni kupona kwako, na pia kuna watu wanaumwa ugonjwa unaofanana na wewe wao wanakuja tu kidogo wakiombewa wanafunguliwa na kutoa ushuhuda, kwasababu liko tatizo kwako ndo maana hupokei ujihudhurishapo mbele za Mungu.

Mungu anataka ufike mahali usiende kwenye uwepo wake kimazoea lazima ujue kwamba kuna viwango vipya naviingia kila niendapo mbele za Mungu. Musa alipo kuwa anarudi kutoka mlimani mbele za Mungu, maisha yake yalibadilishwa, akawa anang’aa, hadi watu wakaogopa kumwangalia usoni pake, huwezi uakaenda mbele za Mungu na maisha yako yakawa vilevile ipo nguvu ya mabadiliko.

MAANDALIO YA MOYO.

Watu wengi walichokosa ni maandalizi, wanakwenda mbele za Mungu pasipokujiandaa, ndiyo maana hata wakienda hawapokei miujiza yao.


Mithali 16:1
"Maandalio ya moyo ni ya mwanadamu. Bali jawabu la ulimi latoka kwa Bwana."

Sikuzote katika maisha ili mambo ya mtu yaende vizuri yanategemeana na maandalizi aliyoyafanya, kama mtu anaharusi ili arusi yake iwe nzuri itategemeana na maandalizi yake, waweza kujiandaa kwa muda mrefu lakini tukio likawa la muda mfupi, harusi inayofanyika kwa siku moja inaweza ikaandaliwa mwaka mmoja, au zaidi, mtihani unaoufanya kwa siku moja unaweza ukajiandaa kwa mwezi zaidi ya mmoja. Kumbe lipo jawabu la Mungu kwa mtu anaye jiaanda vizuri anapohuria mbele za Bwana.Mungu anajibu sawasawa na maandalizi yako, ndiyo maana wengine wanapokea na wengine hawapokei.Uendapo mbele za Bwana moyo ndiyo unaopokea, Mungu akifika anaagalia moyo wa nani umejiandaa kupona, huo uliojiandaa kupona ndiyo unaopona, moyo wa nani umejiandaa kubarikiwa ndiyo unaobarikiwa, kama moyo wako haujajiandaa vhochote Mungu akufanyii chochote, maana Mungu ni Mungu aangalie moyo wa mtu na wala si umbo la nje na ndoomaana habagui kila mtu anampa kulingana na moyo wake ulivyojiandaa.

0 comments:

Post a Comment

Categories

Powered by Blogger.

Popular Posts