Watu wengi wanajiuliuliza nguvu ya Mungu ni nini na inawezeje kutenda kazi? Ni kwamba nguvu ya Mungu ni uwezo wa Mungu ambao unaachiliwa kwa Neno la Mungu na kuleta matokeo kama lilivyoagizwa na Mungu mwenyewe,matokeo ya Neno la Mungu ndiyo nguvu ya Mungu,kwasababu neno likitumwa linaleta mabadiliko kwenye maisha ya watu,na wengine pia wanajiuliza kwamba kuna kuguswa na nguvu ya Mungu hivi huko kuguswa kuna maana gani ?
MAANA YA KUGUSWA
Kugusa ni ishara ya kuonyesha ili mtu akuonyeshe kitu anagusa ili kukudhibitishia,kukupa uhakika wa kile ambacho anakwambia,hivyo Mungu anatabia hii ya kugusa watu wake ili awadhibitishie kwamba yeye ndiye Mungu mafano inasema.
Yeremia 33:3
“niite nami nitakuitikia na kukuonyesha mambo makubwa magumu usiyoyajua” (anaposema kuonyesha ndiyo ishara ya kugusa)
Kumbe hili neno unaweza kuliweka hivi:Niite nami nitakuitikia na kukugusa katika matendo makubwa magumu usiyo yajua,matendo makubwa magumu ndiyo matokeo ya nguvu ya neno la Mungu,hayo matokeo ya nguvu ya neno la Mungu ndiyo uponyaji,hiyo ndiyo mipenyo ambayo Mungu anaachilia kwenye maisha ya watu wake,unaweza ukawa na tatizo unahitaji kuguswa tu na nguvu ya Mungu maana yenyewa ikikugusa tu mabadikliko yanatokea kwenye maisha yako tuone mifano michache kwenye maandiko ya watu walioguswa na nguvu ya Mungu.
1) Vipofu wawili waliomfuata Yesu alipokuwa akipita.
Mathayo 9:27-30
“Yesu alipokuwa akipita kutoka huko,vipofu wawili wakafuata wakipaza sauti,wakisema urehemu mwana wa Daudi.Naye alipofika nyumbani wale vipofu walimwendea Yesu akawaambia mnaamini kwamba naweza kufanya hili? Wakamwambia Naam Bwana,ndipo alipogusa macho yao akawaambia kwa kadili ya imani yenu mpate,macho yao yakafunguka”.
Kipofu ni mtu asiyeona mbele yake anaona giza,hawa vipofu wawili wanafananishwa na watu wasiokuwa na maono ambao hawana uhakika na maisha yao,hawajui walikotoka kupoje wala wanako elekea kuna hali gani? Hivyo wanaishi maisha ya kupapasa,Yesu aligusa macho yao maana yake aligusa maono yao.Nguvu ya Mungu inapojidhihirisha mahali inashughulikia maono.Mwingine yupo kwenye ndoa kwa Muda mrefu hajapata mtoto ukiangalia mbele yake anaona giza kwamba hawezi kupata mtoto,Yesu akikugusa unapata maono ya kupata mtoto,kwasababu ili shetani akupate anakuharibia maono yako na ndiyo maana vijana wengi wanaangamia kwa kukosa maono,wana macho lakini hawaoni maana maono ndiyo macho yanayobadilisha maisha ya mtu.Kumbuka nguvu ya Mungu ikimgusa mtu inashughulikia maono ya mtu,chochote unachokitaka kwa Mungu ni lazima ukione kwanza ndipo ukipate,ukiona maisha mazuri yatakuja maisha mazuri,ukiona kupona utapona,Yesu aligusa macho yakafunguka,nguvu ya Mungu ikikugusa utaona kule unakoelekea.
1) Mama mkwe wa Petro amelala hawezi homa imemkamata.
Mathayo 8:14-15
“Hata Yesu alipofika nyumbani kwa Petro,akamwona mkwe wa Petro,mamaye mkewa maelala kitandani hawezi homa.Akamgusa mkono homa ikamwacha,naye akaondoka akawatumiakia”
Umejiuliza kwanini ?Yesu aligusa mkono homa na ikamwacha,kwanini? nguvu ya Mungu iligusa mkono wa Mama mkwe wa Petro homa ikamwacha,kumbe kuna kitu Yesu alikuwa anakishughulikia kwenye mikono ya mama mkwe wa Petro,mikono inahusika na utendaji wa kazi(kila kazi ianafanywa na mikono).Angalia sana kuna watu wengine mikono yao imebeba laana kila wanachokifanya hawafanikiwi mpaka wanapata homa,magonjwa kutokana na mkandamizo wa mawazo wakutokufikia malengo yao kama mama mkwe wa Petro,kumbuka kwamba biashara zako ni kazi ya mikono,masomo yako ni kazi za mikono,kilimo chako ni kazi za mikono na maandiko yanasema Mungu atabariki kazi za mikono,Yesu alipokuwa anagusa mikono ya mama mkwe wa Petro alikuwa anashughulikia laana iliyokuwepo kwenye mikono ya mama mkwe wa Petro.Mwambie Yesu kama alivyogusa mikono ya Mama mkwe wa Petro mwili wake ukawa salama vivyo hivyo akuguse na wewe kazi zako zikawe salama.
MAMBO MUHIMU YA KUFANYA ILI UGUSWE NA NGUVU YA MUNGU
1)Viguse vilivyo mgusa Yesu.
Marko 5:25-34
“Na mwanamke mmoja mwenyekutokwa damu kwa muda wa miaka kumi na miwili,na kuteswa mengi kwa mikono ya matabibu wengi,amegharimia vitu vyote alivyonavyo, kusimfae hata kidogo bali hali yake ilizidi kuwa mbaya bali aliposikia habari za Yesu,alipitaa katika mkutano kwa nyuma akaligusa vazi lake,maana alisema nikiyagusa mavazi yake tu nitapona,mara chemchemi ya damu yake ikakauka,mara akafahamu nafsini mwake kwamba amepona msiba ule,na mara Yesu hali akifahamu nafsini mwake ya kwamba nguvu zimemtoka,akageuka kati ya mkutano,akasema ni nani aliyenigusa? wanafunzi wake wakamwambia Je wawaona mkutano wanavyo kusongasonga,nawe wasema ni nani aliye nigusa.akatazama pande zote ili amwone yeye aliyetenda neno hilo.Yule mwanamke akaingiwa na hofu na kutetemeka,akijua lililompata,akaja akamwangukia,akamweleza kweli yote,Akamwambia binti imani yako imekuponya,enenda zako kwa amani uwe mzima,usiwe na msiba wako tena."
Kuna nguvu katika kuvigusa vilivyomgusa,ili nguvu ya Mungu ikuguse kanuni mojawapo ya kiroho ni kugusa vilivyomgusa,mwanamke mwenye kutokwa damu aligundua hii kanuni ya kiroho akagusa upindo wa mavazi yake Yesu,nguvu zikamtoka Yesu kupitia kwenye mavazi zikamgusa mwanamke.Huyu mwanamke alitengwa na jamii yake kwasababu ya kutokwa damu na alilipa gharama ya damu kumwagika,kwa kuzunguka mahospitalini na kukutana na waganga wa kila namna lakini ugonjwa wake haukupona,ila alipopata habari za Yesu alisema nikiyagusa mavazi yake tu nitapona,angalia vizuri mavazi yalikuwa yamemgusa Yesu kile kitendo cha kugusa kilicho mgusa nguvu ya Mungu ikamfungua mwanamke,kumbuka mwanamke hakugusa ngozi bali vazi la Yesu.Vazi la Yesu limepewa nafasi ya kugusa ngozi ya Yesu ndilo limebeba nguvu inayobadilisha,na unapogusa vazi la Yesu automatically nguvu zinamtoka Yesu na kukugusa,unaweza ukawa unasema mbona naingia kanisani ila ugonjwa wangu hauponi swali ni kwamba umevigusa vilivyomgusa? Na ndiyo maana wengine wakiomba kidogo Mungu anasikia maombi yao na kuyajibu kwasababu wamevigusa vilivyomgusa hata ndani ya kanisa tutaendelea kutofautiana katika wengine watafanikiwa sana na wengine watafanikiwa kidogo kwasababu ya kutofautiana katika kuvigusa vilivyo mgusa,wataingia wagonjwa watatoka wagonjwa na wengine wazima.Hata siku ile mwanamke hakuwa mgonjwa peke yake,walikuwepo wengi lakini aliyegusa vilivyomgusa ndiye aliyefunguliwa.
Luka 6:16
“Na makutano wote walikuwa wakitaka kumgusa,kwasababu uweza ulikuwa ukimtoka ukiwaponya wote."
Je unataka uweza wa Mungu ukifikie? mguse ili ukufikie hawa walikuwa wakimgusa na uweza wa Mungu ulikuwa ukimtoka na kuponya magonjwa yao.Watu wengi wanapenda kuombewa lakini hawapendi kulipa gharama ya kugusa vilivyomgusa,hata kama mtumishi wa Mungu anakuombea hakikisha una vigusa kwanza vilivyomgusa Mungu ili maombi yalete matokeo,haijarishi ni tatizo gani wewe gusa tu vilivyomgusa ipo nguvu inayobadilisha katika vile vilivyomgusa Yesu.Mtu anaweza akawa anajiuliza hivyo vitu vilivyomgusa Yesu ni vitu gani? Au hayo mavazi aliyoyagusa mwanamke yalikuwa yanamaanisha nini?,tuangalie kwa undani maana Roho mtakatifu anataka akufundishe kitu.
0 comments:
Post a Comment