VITU
NA WATU WALIOMGUSA MUNGU.
Tunaposema
mwanamke alligusa mavazi ni kwasababu kuna vitu na watu ambao Yesu anawatumia
kama mavazi yake,ikiwa umefanya vitu kwao wakafurahi unaruhusu nguvu ya Mungu
ipitie wao na kubadilisha maisha yako,ninaposema hayo nina maana hii si kila
mtu au kila kitu kimemgusa Mungu,kwamaana hii kuna wengine unaweza ukawagusa kama
vazi la Yesu na nguvu za Mungu zisikuhudumie lakini kuna vitu na watu wengine
wao wamegusa ngozi ya Yesu ukiwagusa hao hutokuwa kama vile ulivyokuwa ambao ni:
i. Watumishi wa
Mungu.
Watumishi
wa Mungu ni mavazi ya Yesu ndiyo waliomgusa Yesu wao wamebeba mabadiliko ya
maisha yako ninaposema kugusa nina maana hii ukionesha kuwajali, kula pamoja nao,watu wengi wanatamani kuguswa
na nguvu ya Mungu wakiwa wamesahau kwamba.
1Wafalme
17:13-16
“Eliya akamwambia usiogope,enenda
ukafanye kama ulivyosema,lakini unifanyie kwanza mkate mdogo uniletee,kisha
jifanyie nafsi yako na mwanao.Kwakuwa Bwana Mungu wa Israeli asema hivi,lile
pipa la unga halitapungua wala ile chupa ya mafuta haitaisha,hata siku ile
Bwana atakapoleta mvua juu ya nchi,Basi akaenda akafanya kama allivyosema
Eliya,na yeye mwenyewe na Eliya na nyumba yake wakala siku nyingi.Lile pipa la
unga halikupunguka wala ile chupa ya mafuta haikuisha,sawasawa na neno la Bwana
kwa kinywa cha Eliya”
Mungu alitaka kubadilisha maisha ya
mwanamke mjane maana alikuwa amekata tamaa kwasababu ya njaa ya kipindi kile
lakini kanuni ya kiroho inasema uviguse vilivyomgusa.Eliya mtumishi wa Mungu
alikuwa amemgusa Mungu katika utumishi wake hivyo alikuwa ni vazi la Mungu
mwanamke mjane alipofuta njaa kwa Eliya naye Mungu akafuta njaa kwa mwanamke
mjane,unapobadilisha maisha ya watumishi wa Mungu naye Mungu anabadilisha
maisha yako maana wao wamemgusa Mungu,mwingine anaweza kusema mbona ninacho kidogo
mwanamke mjane hakuwa nacho kingi ila alitoa kwa imani na Mungu akatengeneza mipenyo.
Si mwanamke mjane tu hata mwanamke
mshunemu ambaye alikuwa tasa hazai,lakini alimpokea Elisha na kumpa chakula
nakumfanyia kitanda kizuri kwaajili ya kulala bali Elisha ni mtumishi wa
Mungu,vazi la Mungu amemgusa Mungu katika utumishi wake,alipompokea Elisha naye
akapokea mtoto(2wafalme 4:8).Kumbuka
kitendo cha mwanamke kugusa upindo wa vazi la Yesu msiba wake ulipona Gusa
vilivyomgusa.
Hata
Ibrahimu Baba wa imani alikuwa amehaidiwa na Mungu kupata mtoto kwa muda mrefu
sana lakini asipate,siku moja aliwapokea watumishi wa Mungu walipopita karibu
na hema yake na kuwanawisha miguu na kuwapa chakula walitamka kitu kwake “Mwaka kesho wakati kama huu utapokea mtoto”(Mwanzo
18:1-10) akampokea Isaka,wapo wengi waliogusa vilivyomgusa na maisha yao
yakabadilishwa,Mungu nataka akuguse na nguvu yake gusa kwanza vilivyo mgusa.
i.Makanisa
na huduma
Makanisa
na huduma mbali mbali ni vitu vilivyomgusa Yesu unapogusa ni lazima maisha yako
yabadilishwe,Sulemani alimjengea Mungu nyumba,kwasababu alikuwa amegundua siri
hii kwamba nyumba ya Mungu imefungamanishwa na nguvu ya Mungu na alikuwa
anataka ufalme wake uwe imara alimjengea Mungu nyumba,haijawahi kutokea katika
Israeli mtu aliyekuwa kama Sulemani katika ufalme wake kipindi chake hakujawahi
kutokea vita,alikuwa na mahali nyingi kupita
wafalme wote duniani,alikuwa na hekima isiyoelezeka kwasababu alimjengea
Mungu nyumba,angalia makanisa yanayojengwa toa mchango wako uone kama nguvu ya
Mungu haijakugusa siyo mpaka mchango utangazwe kanisani ndipo ufanye uonapo tu kuna upungufu fanya haraka
ili Mungu aachilie nguvu ya kukugusa,angalia ndani ya kanisa ukiona jengo
limechakaa angalia washirika utawaona nao pia wamechakaa,ukikuta kanisa limejengwa
vizuri limepambwa utakuta pia washirika
wanamaendeleo kwenye maisha yao.Kwanini? ni kwasababu watu wengi hawajaigundua
siri hii.
Na
hata wakati mmoja wazee wa Israeli walimwendea Yesu kwa kumtaka amponye mtumwa
wa akida mmoja ambaye alikuwa hawezi,ili maombi yao yajibiwe yawe na ushawishi
mbele za Yesu,walionyesha kile alichokifanya kwenye lile taifa,wakasema alitujengea na Sinagogi Yesu akapata
ushawishi kwenda kumponya(Luka 7:1-6) unaweza
ukawa unataka uponyaji lakini hauja ushawishi ufalme wa Mungu uachilie nguvu
yake,wanao jenga makanisa nakusapoti huduma mbalimbali wanakuwa wamegusa
vilivyogusa ufalme wa Mungu hivyo nguvu za Mungu zinapita kwenye huduma na
kugusa maisha yao,labda hauna kazi,au unafanya biashara bila faida bali unaona
madeni yanakuwa mengi,ukiona kunaujenzi wa kanisa nenda ukachangie ili uone
kanuni hii ya kiroho inavyofanya kazi.
i.Yatima,wajane
na mgeni pamoja na maskini.
Watu
wengi hawajajua kwamba yatima na wajane,wageni pamoja na maskini wao ni maskini
wao ni mavazi ya Yesu kwamba ukimaliza shida zao naye Yesu anamaliza za
kwako,kumbuka kile kitendo cha mwanamke mwenye kutokwa damu kugusa upindo wa
vazi la Yesu nguvu za Mungu zikamhudumia,Je umewahi kuapata historia ya
mwanamke Dorkasi ambaye aliumwa mpaka akafa,kipindi cha uhai wake alikuwa
anawajali wajane,angalia mstari huu.
Matendo 9:39.
“Petro akaondoka akafuatana
nao,alipofika wakampeleka juu orofani wajane wote wakasimama karibu
naye,wakilia na kumwonyesha zile kanzu na nguo alizoshona Dorkas wakati ule
alipokuwa pamoja nao”
Soma na uelewe tabia ya mavazi
ya Yesu ,hawa wajane walisimama kama mavazi ya Yesu,wakatoa sauti za kilio,vile
vilivyomgusa Yesu vina sauti inayogusa nguvu inayogusa kwa wakati huo Dorkasi
alikuwa hajililii lakini wajane walilia(mavazi yalilia)unaweza ukapita kwenye
hali ngumu kwa kiwango ya kwamba ukashindwa kujiombea mwenyewe lakini vile
ulivyowahi kuvigusa vilivyomgusa Yesu vikatoa sauti kwaajili yako,kufufuka kwa
Dorkas hakukuwa kwa sababu Petro anaoupako wa kufufua wafu ila ni kwasababu
Dorkasi amegusa vilivyomgusa.
Mambo ya walawi 19:9-10
“Na mtakapovuna mavuno ya nchi
yenu,usivune kabisa kabisa pembe za shamba lako,wala usiyakusanye masazo ya
mavuno yako.Wala usiyakusanye masazo ya mizabibu yako yaliyopukutika uyaache kwaajili
ya maskini na mgeni,mimi ndimi Bwana Mungu wako”
i. Wazazi(Baba na
Mama)
Wazazi
ni mavazi ya Yesu wamegusa ngozi ya Yesu,hivyo wamefungamanishwa na nguvu ya
Mungu,kuna mahali huwezi kufika ukiwa hujafanya kitu kwao,watu wengi
wamefanikiwa lakini ukiangalia wazazi wao wanaishi katika hali
mbaya,shida,umaskini, hawajui ya kwamba masononeko ya wazazi wao ni mikosi
kwenye maisha yao,ili nguvu ya Mungu ikuguse nilazima uviguse vilivyomgusa hii
ndiyo kanuni ya kiroho.Isaka alipoona kwamba umri wake umekwenda na macho yake
yamepofuka akatakakumbariki mwanawe Esau lakini Isaka Babaye alijua kanuni ya
kiroho kwamba Esau asipo vigusa vilivyomgusa hawezi akapokea Baraka za
wazazi,hivyo akamwagiza amtengenezee chakula kitamu namna ile anapenda.
Mwanzo
27:3-4
“Basi naomba chukua mata yako,podo lako
naupinde wako,ukaende nyikani uniwindie mawindo.ukanifanyie chakula kitamu
namna ile nipendavyo,ukaniletee ili nile Roho yangu ikubariki kabla sijafa”
Wazazi wako wanataka ufanye kitu kwao kabla
hawajafa,wengine wazazi wao wanaishi kwa shida na huku uwezo wanao ila wakifa
wanapamba vizuri majeneza ilikuwaonyesha kwamba wanawajali,usijali maiti
iliyokufa wajali wazazi wako wakiwa hai ili nguvu ya Mungu ikuguse,Isaka
alimwambia shituka Esau nguvu za Mungu haziwezi kukugusa nikiwa nimekufa hata
ukinifanyia jeneza zuri kiasi gani nikiwa hai fanya chakula kitamu kama
nipendavyo nikubariki.Huwezi kupiga hatua yoyote kwenye maisha yako kama
hujafanya kitu kwa wazazi wako,naye mtume Paulo hawi mbali kwamba kuna watu
wanakufa leo kwasababu hawaaeshimu wazazi wao.
Waefeso 6:2-3
“Waheshimu Baba yako na Mama yako;amri
hii ndiyo amri ya kwanza yenye ahadi,upate heri ukae siku nyingi katika dunia”
Ni ukweli Mungu amehaidi kwamba miaka yetu ni
sabini au tukiwa na nguvu themanini lakini ahadi hiyo ili itimie kwako ni
lazima kwanza uviguse vilivyomgusa wazazi ukiwaheshimu wamefunga manishwa na nguvu
yakuwafanya watu waishi maisha marefu.Kuna ndugu mmoja alikuafa.Kipindi cha
uhai wake alikuwa na kazi yake nzuri,nyumbani kwake alikuwa amejijenga sana
lakini alikufa katika umri mdogo sana hata miaka 30 hakufikisha,siku ya mazishi
yake ilipofika walienda kumzika mahali alipozaliwa,watu walipotazama maisha ya
wazazi wake,maana wazazi wake mahali tu wanapolala,nyumba wanayoishi imejengwa
kwa mianzi na kila mmoja akawa anashangaa kwamba yeye aliishi kwenye maisha ya
kifahari ia wazazi wake wanaishi kwenye maisha kama haya si angewabadilisha na
wazazi wake?kumbe ndiyo maana amewahikufa,unapofanikiwa usiwasahau wazazi wako
iliusiondoke mapema duniani wazazi wamebeba Baraka ya maisha marefu,namna
unavyowagusa kwakufanya namna wanavyopenda wao,unakuwa sawasawa na mwanamke
mwenye kutokwa damu alipovigusa vilivyovyomgusa Yesu aliongeza maisha ya kuishi
duniani pamoja na kwamba alikata tamaa.